‘Hii ni imani ambayo nimeifikiria
muda mrefu na nikajua lazima niifate, kila mtu ana kitu ambacho anakiamini na
kwangu naamini moto ndio kila kitu kwenye maisha, kama maandiko yanavyosema
Mungu ni moto ulao… naamini moto ndio mfumo ambao hata Mungu anatokana na moto
wenyewe‘ – Afande Sele
Kwenye sentensi ya pili Afande amesema ‘wakisema Mungu hajulikani au Mungu
hujui ni kitu gani hapo kwangu siwezi kuamini kitu ambacho hakionekani kwa hiyo
mimi naamini Mungu ni lile jua linalowaka sababu ndio moto mkuu kuliko mioto
yote,sasa
kama Mungu ni moto ulao basi mimi napaswa niliwe na moto ule‘
‘Naamini nikichomwa
moto nitakua majivu, unaposema Mungu ni moto ulao inamaana mimi moja kwa moja
nitakua nimeliwa nimeingia ndani ya Mungu mwenyewe, hata kesho nikifariki
nikachomwa moto nikawa majivu, sipendi kufufuliwa kwenye mazingira ya
ubinaadamu tena sababu nimegundua ubinaadamu sio kitu kizuri cha kujivunia‘
‘Japo binadamu
wanaweza kujivunia sababu ndio wanatengeneza Ndege, Magari na vitu vingine….
binadamu ndio kiume mbaya na muovu, msaliti, mnafiki, batili kuliko kiumbe
chochote katika ulimwengu, hata dunia yenyewe itamalizwa na binadamu na sio
kiumbe mwingine kwahiyo ili kuukana huu ubinadamu sipaswi kuzikwa kwenye
udongo, nikizikwa kwenye udongo manake nitafufuliwa kama binadamu tena kitu
ambacho sikitaki‘
– Hayo
ni maneno ya Afande Sele msanii wa siku nyingi kwenye muziki wa bongofleva
Kwa
kumalizia, Afande amesema ‘Mungu ninaemwamini
mimi ni moto na moto mkuu kuliko yote ni jua hata samaki anayeishi chini ya
bahari kabisa jua likiwaka asubuhi anatoa mgongo juu inamaana anatoa heshima
yake kwa Mungu, hiyo ndio imani yangu na wala simlazimishi mtu mwingine yeyote
aamini ninavyoamini mimi, hata familia yangu na watoto wanajua baba akifa
anatakiwa kuchomwa moto’
Ukitaka
kufahamu zaidi aliyoyasema Afande Sele tazama hii video hapa chini…
CHANZO NI Millardayo.com
0 maoni:
Post a Comment