Baada ya kukutana na Rais Xi Jinping wa
China, Rais Barack Obama amesema wote wanawajibu wa kulifanya eneo hilo la rasi
ya Korea kuwa eneo huru lisilo na nyuklia na kuiweka vikwazo zaidi dhidi ya
Pyongyang.
Hali ya wasiwasi imetanda juu ya jaribio
la Korea kaskazini kuendelea silaha za nyuklia na majaribio yake ya teknolojia
ya makombora.
Awali Rais Obama alikutana na viongozi
wa Japan na Korea kusini kuweka msimamo wa pamoja juu ya suala la usalama
katika rasi hiyo ya Korea.
Pamoja na kwamba nchi ya pili kwa nuklia
duniani Urusi haijahudhuria mkutano huo, Rais Obama alifanya mazungumzo na Rais
Xi Jinping of China ambapo amesema yeye pamoja na Rais XI wamekubaliana kuondoa
nuklia katika eneo la rasi ya Korea na kutekeleza vikwazo vipya vilivyopitishwa
na Umoja wa Matiafa kwa lengo la kuipa shinikizo jipya Korea Kaskazini.
Kwa upande wake Rais Xi amesema China
inataka kuongeza mawasiliano na kuratibu jambo hilo ambapo nchi zote mbili
zimekubaliana kukutana kila mwaka kuzungumzia masuala ya usalama wa nyuklia.
Wamesema pia watafanya kazi kwa pamoja
kuzuia malighafi za kutengeneza nuklia na kuratibu juhudi za kuzuia malighafi
hizo kuangukia mikononi mwa magaidi.
Hata hivyo kasoro moja katika mkutano
huo ni kutokuwepo kwa Rais Vladimir Putin. Urusi na Marekani wanamiliki karibu
asilimia 90 ya silaha za nyuklia hivyo Mosco kukataa kuhudhuria mkutano huo
unaweza kufanya makubaliano yatakayofikia isiyatekeleze.
Kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment