MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

India watu wapewa likizo kwa sababu ya filamu mpya ya mwigizaji Rajinikanth

160722051210_rajinikanth_640x360__nocredit
Wafanyakazi wengi kusini mwa India leo wamepewa likizo kwa sababu ya filamu mpya inayoanza kuonyeshwa kwenye kumbi za sinema leo.Filamu hiyo ni ya mwigizaji nyota wa asili ya Tamil, Rajinikanth.
Hatua hiyo imechukuliwa kuzuia watu kutumia visingizio kama vile kwamba wanaugua ili wasifike kazini.
Inahofiwa wengine huenda hata wangezima simu zao au kutofika kazini bila kueleza sababu.
Filamu hiyo kwa jina Kabali inaonyeshwa katika kumbi 12,000 za sinema leo.
Rajinikanth, ni mmoja wa waigizaji wanaolipwa pesa nyingi sana bara Asia na mmoja wa waigizaji mashuhuri zaidi kutoka India.
Hata kabla ya kuzinduliwa, filamu hiyo ya Kabali, ambayo inaangazia uhalifu wa magenge, imejizolea $30m (£20m) kupitia mauzo ya haki zake.
Itatolewa pia kwa lugha za Kitelugu, Kihindi na Kimalay.
Katika miji kama vile Chennai na Bangalore, baadhi ya kampuni zimetangaza Ijumaa kuwa siku ya likizo na hata kuwapa wafanyakazi tiketi za bure wakatazame filamu hiyo.
Kampuni moja inasema imechukua hatua hiyo kuzuia watu kufika kwa wingi wakiomba likizo siku ya leo.
Rajinikanth mwenye umri wa miaka 65, ameigiza katika filamu zaidi ya 170, nyingi katika lugha ya Kitamil.
Source: BBC
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment