MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Manaford: Hakuna mzozo kampeni ya Trump

Donald TrumpImage copyrightGETTY IMAGES
Image captionDonald Trump amekuwa akishutumiwa kwa kauli zake
Msaidizi kuu wa Donald Trump amekana taarifa kuwa kuna mgawanyiko mkubwa kwenye Kampeni baada ya kile kinachodaiwa mfululizo wa kauli za mgombea wa Chama cha Republican, zenye kukwaza.
''Kampeni ziko vizuri, tumejipanga, tunasonga mbele,'' Paul Manaford ameiambia Fox News.
Vyombo vya habari vya Marekani viliripoti kuwepo kwa mvutano baada ya Trump kurejea matamshi yake ya kushambulia wazazi wa Mwanjeshi aliyeuawa nchini Iraq.
Baadhi ya Maafisa wa Kampeni za Trump wamesema ''wanahisi kuwa wanapoteza muda wao''
Hata hivyo, Manafort amemlaumu mpinzani wa Trump wa Chama cha Democrat, Hillary Clinton kwa ripoti hizo
''Hii ni kauli nyingine ya Clinton ambayo imebebwa na vyombo vya habari, amesema ''Bwana Trump amejitokeza wiki hii kwenye mikusanyiko mikubwa sana ya watu walifurika mpaka mtaani''
Siku ya Jumatano Trump aliandika kwenye anuani yake ya Tweeter kuwa ''kuna umoja kwenye Kampeni yaangu, pengine mkubwa zaidi kuliko siku zote''.
Vita vyake vya maneno na Khizr na Ghazala Khan, wazazi wa Kapteni Humayun Khan aliyeuawa nchini Iraq, vimesababisha watu kutofautiana ndani ya Chama cha Republican.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment