MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Olimpiki Rio 2016: Kina dada wa Zimbabwe wacharazwa 6-1

Olimpiki Rio 2016Image copyrightAP
Image captionSweden walilaza Afrika Kusini kupitia bao la Nilla Fischer kipindi cha pili
Timu ya taifa ya kina dada ya Zimbabwe imecharazwa 6-1 na timu ya taifa ya Ujerumani kwenye mechi zilizochezwa siku ya kwanza ya michezo ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro, Brazil.
Ujerumani, waliokuwa mabingwa 2000, 2004 na 2008, walikuwa na kibarua rahisi dhidi ya timu hiyo ya Afrika. Wakati mmoja, mabao yalikuwa 2-1 lakini mabinti hao wa Zimbabwe walionekana kulemewa na uchovu dakika za mwisho mwisho na wakabebeshwa magoli matatu katika kipindi cha dakika 16.
Sweden waifunga Afrika KusiniImage copyrightAP
Image captionWachezaji wa Sweden baada ya kuifunga Afrika Kusini
Michezo ilianza kwa mechi kati ya Sweden na Afrika Kusini ambapo Sweden walishinda 1-0.
Baadaye, wenyeji Brazil walilaza Uchina 3-0. Uwanja wa Olimpiki, wenye uwezo wa kupokea mashabiki 60,000, ulikuwa hauna mashabiki wengi mechi ya kwanza, lakini zaidi walifika kabla ya mechi hiyo ya Brazil.
Janine Beckie wa Canada naye alifunga bao sekunde 20 pekee baada ya mechi yao dhidi ya Australia kuanza, na kuweka rekodi ya bao la kasi zaidi lililofungwa katika historia ya soka ya wanawake Olimpiki.
Marekani wanapigiwa upatu ksuhinda michuano hiyo.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment