Mzee mmoja wa miaka 62 amekamatwa baada ya kuweka tindi kali katika chupa ya mafuta ya kulainisha kwa kiingereza 'Lubricant' katika kilabu ya ngono nchini Australia.
Hakuna majeraha mabaya yalioripotiwa katika kisa hicho katika kilabu ya Aarrows ambayo ni ya wapenzi wa jinsia moja.Vifaa katika chumba hicho viliwekwa kengele ya kupiga kamsa baada ya kuharibiwa hapo mbeleni.
Mshukiwa huyo alishtakiwa na makosa ya kuweka sumu kwenye chupa hiyo kwa lengo la kutaka kujeruhi ama kuumiza.
Msemaji wa polisi ameambia gazeti la Daily Telegraph nchini Australia kwamba wachunguzi hawajabaini lengo la hatua hiyo na kwamba hakuna ishara ya kuwepo kwa chuki.
Mshukiwa aliwachiliwa kwa dhamana na anatarajiwa kufikishwa mahakamani mnamo terehe 20 mwezi Septemba.
Kilabu ya Aarows hujitangaza kuwa eneo la kujivinjari ambapo ngono salama hukubalika licha ya jinsia.
0 maoni:
Post a Comment