Vikosi vya usalama vimevamia makao makuu ya chama cha mgombea urais aliyeshindwa Jean Ping.
Msemaji wa serikali alisema kuwa oparesheni hiyo kwenye mji mkuu Libreville ililenga kuwafurusha wahalifu.Alisema wao ndio walihusika katika kuchomwa kwa majengo ya bunge siku ya Jumatano.
Bwana Ping alisema kuwa watu 2 waliuawa wakati wa uvamizi katika makao makuu ya chama.
Mapema wafuasi wake waliinga barabarani kupinga tangazo kuwa rais Ali Bongo alishinda uchaguzi kwa chini ya kura 6000.
kutoka BBC Swahili
0 maoni:
Post a Comment