MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Waasi watishia kutoshiriki mazungumzo ya amani Syria

Waasi watishia kutoshiriki katika mazungumzo ya amani yanayosimamiwa na Urusi na Uturuki
Image captionWaasi watishia kutoshiriki katika mazungumzo ya amani yanayosimamiwa na Urusi na Uturuki
Makundi kadhaa ya waasi nchini Syria yamesema kuwa yamesimamisha mashauriano ya kupanga mkutano wa amani unaoandaliwa na Urusi na Uturuki kufanywa katika nchi ya Kazakhstan mwezi huu, yakilaumu Serikali kwa kuvunja mapatano ya kusitisha mapigano kwa siku nne.
Waasi hao wanasema walikuwa wameheshimu mapatano hayo lakini wanajeshi wa serikali ya Syria na washirika wao wa Irani wamekiuka mwafaka huo mara kadhaa.
Waasi hao wanasema maeneo yaliyoshambuliwa bila kujali ni kama vile Ghouta na Wadi Barada, maeneo hayo yote yakiwa karibu na Damascus.
Waasi hao wanashikilia Wadi Baradi, ambalo ni eneo muhimu sana kwa maji yanayowashughulikia wakaazi wa Damascus.
Waasi wamelaumu Serikali kwa kuyachafua maji kwa kutumia dizeli.

kutoka BBC Swahili
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment