MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Watu 20 wafariki kutokana na baridi kali Ulaya

PugliaHaki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionBaadhi ya maeneo ya kusini mwa Italia yamefunikwa na theluji, unaweza ukafikiria ni Siberia
Watu zaidi ya 20 wamefariki kutokana na baridi kali ambayo imeendelea kukumba maeneo mengi ya Ulaya.
Watu kumi walifariki kutokana na baridi hiyo kali Poland siku ya Jumapili.
Miili ya wahamiaji watatu, wawili kutoka Iraq na mmoja kutoka Somalia, ilipatikana karibu na mpaka wa Uturuki na Bulgaria.
Vifo pia vimeripotiwa Italia, Jamhuri ya Czech na Ukraine.
Safari nyingi za ndege pia zimesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa.
Nchini Uturuki, mlango wa bahari wa Bosphorus umefungwa na meli haziruhusiwi kupita kutokana na dhoruba kali ya theluji.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment