MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Mwanamke ajuta kumtia nyoka katika ndewe yake

Mwanamke amtia nyoka katika ndewe yake
Mwanamke mmoja kutoka jimbo la Oregon alifanikiwa kumuingiza nyoka wake katika ndewe kabla ya nyoka huyo kukwama.

Ashley Glawe alichapisha picha yake katika mtandao wa facebook akiwa hospitali.
Aliandika: Kilikuwa kisa cha kushangaza sana katika maisha yangu baada ya nyoka wangu kuingia katika tundu ya sikio langu .

Alichapisha katika ujumbe huo katika mtandao akisema anamshikilia nyoka huyo kwa jina Bart baada ya kuingia katika ndewe yake ya sikio.

''Lilikuwa tukio la haraka hadi sikuweza kujitetea''Nyoka aliyeingia katika ndewe na kukwama
Anasema kuwa ana wasiwasi mkubwa kuhusu nyoka wake lakini hakuna tatizo lolote kufikia sasa.
Aliwaambia marafiki zake mtandaoni kwamba madaktari walidunga sindano sikio lake na kulituliza, wakapanua ndewe hiyo kabla ya kumtoa nyoka huyo.
Nyoka huyo kwa sasa anadaiwa kuwa kati hali nzuri.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment