Wema Sepetu anataka kuweka jambo moja ‘very clear’ kuwa yeye si mtumiaji wa madawa ya kulevya.
Staa huyo ametoa kauli hiyo baada ya kuwepo kwenye orodha ya mastaa
wanaotuhumiwa kubwia unga na walioamriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda kujisalimisha kituo cha polisi central jijini Dar,
Ijumaa hii kwa mahojiano zaidi.
“Mimi kama Wema nimekuwa nikisemwa sana kuhusu kujihusisha na
utumiaji wa madawa ya kulevya na hata kujihusisha katika kuuza madawa ya
kulevya,” amesema Wema kupitia app yake.
“Sometimes wanasema nimefungwa, sometimes nimenyongwa, sometimes
nimekamatwa hususan pindi ninaposafiri kwenda nchi mbalimbali, na sasa
hivi nimeambiwa kwamba natumia madawa ya kulevya. Well, ni habari ambazo
mheshimiwa mkuu wa mkoa amesema hana uthibitisho nazo lakini amelazimu
kutaja majina kadha wa kadha ambayo ndio hivyo ameyataja mengine kwenye
vyombo vya habari, na ameamuru twende tukaripoti kesho (leo Feb 3),
ifikapo saa tano asubuhi,” ameongeza.
“Mi nasema hivi, nitaenda, nitaripoti, kwasababu ni wito ambao
ametaja mkuu wa mkoa wangu kuona amefanya, unaambiwa kubali wito,
usikatae neno. Kwahiyo tutaenda kesho, na ntamsikiliza yale ambayo
anataka kuniambia, iwapo tukishajua which is true, which is not, then
tutajua from there what to do, sasa hivi sina cha kusema, sina cha
kufanya, because bado sijaonana naye, kwa sasa niacheni tu nirelat but I
want to assure you one thing, I am not a drug addict, and I am not a
drug abuser, and if I was nadhani we all know how drug addicts act, we
all know how drug abusers
wanakuwaga. I want you guys to relax, do not
worry, everything is going to be fine.”
Mastaa wengine waliotajwa ni TID, Mr Blue, Chidi Benz, Recho na wengine.
Bongo 5
MWERA AMAZING BLOG
- Blogger Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 maoni:
Post a Comment