Jinsi ya kulinda penzi
lililorudi baada ya kuvunjika
Lengo la ndoa ni kupata kitulizo cha nafsi, akili na mwili, pia kupata
watoto. Ni jambo lisilopendeza kwa ndoa iliyofungwa kwa furaha na matumaini
tele kuvunjika.
Kwa wanandoa walioishi
kwa kupendana lazima watatafakari chanzo cha ndoa yao kuvunjika na hatimaye
kutafuta ufumbuzi wa kurudiana.
Katika mada zilizopita
tumeona sababu za ndoa nyingi kuvunjika. Pia baada ya kuvunjika nilifafanua
njia za kufanya ili kuirudisha ndoa iliyovunjika.
Leo ninawaletea njia za
kufanya ili kulinda penzi lililorudi upya baada ya kuvunjika. Usibandue macho
yako kwenye safu hii ili ufahamu njia hizo.
*************
Mwenyezimungu kutokana na
uwezo wake ametuumba wanaadamu kuwa na kinyongo. Mara nyingi kinyongo humfanyia
yule unayehisi hakukutendea haki. Ni ukweli usiyopingika kuwa, kuvunjika kwa
ndoa kumetokana na mmoja kati ya wanandoa kuwa chanzo, kufanya vitendo ambavyo
mwanandoa mwenziwe hakuridhika navyo.
Hivyo
basi kwa kuwa mmoja kati ya wanandoa ndiye mwenye makosa, ni jambo la kawaida
kuona aloyekosewa kuwa na kinyongo. Ili kuweka mambo sawa na muishi vema kama
au kuliko mlivyokuwa mnaishi awali, nilazima kuyazingatia mambo yafuatayo.
1. Kwanza; Tambua mfumo wa maisha mliokuwa mkiutumia katika maisha yenu
kabla ya kuachana. Baada ya kuutambua, jitahidi kuepuka mambo yaliyozua
mfarakano hapo awali ili yasirudie tena.
2. Jisikie upo huru wakati wote,
ishi bila hofu. Ishi kama hakuna mfarakano wowote uliyotokea baina yako na
mpenzi wako. Ondoa hofu, acha kujihisi.
0 maoni:
Post a Comment