MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG
                      MASWALI NA MAJIBU
Mke wangu anatembea na mpangaji, nifanyeje?
Naam, wapenzi wasomaji wa safu hii ya Mahusiano na Ushauri. Nikiamini wengi wenu mna afya nzuri tangu tulipoachana wiki iliyopita. Kama kawaida yangu, siku kama ya leo, huwa najibu maswali ambayo baadhi yenu mmetuma kwa ujumbe wa simu na wengine kupitia barua pepe. Karibuni.

Mke wangu anatembea na mpangaji, nifanyeje?
Nina mke ambaye nimebaini amenigeuka na sasa anatembea na mpangaji wangu. Mbaya zaidi anamuingiza chumbani mwangu. Nishauri Uncle J, nifanyeje?

JIBU: Mwanandoa kutoka nje si jambo jema hata kidogo. Inatia uchungu kuwa na mume au mke anayetoka nje ya ndoa.

Matukio ya kutembea na wapangaji yapo mengi miongoni mwa wanandoa. Kinachoshangaza kwa mkeo ni kule kufanya hayo ndani ya chumba anachotumia na mwenzake.

Iwapo jambo hili lina uhakika baada ya mwenyewe kujiridhisha, baddala ya kusikiliza maneno ya kuambiwa, fanya uamuzi. Umewahi kumuuliza kuhusu jambo hili? Kama bado muulize ili usikie anasemaje. Akijibu ovyo amua kwa kumrudisha nyumbani kwao. Usimpe talaka haraka japo kosa hili ni zito mno. Anaweza kujirudi.

Ukiona hajabadilika, mpe talaka na utulie kabla ya kutafuta mwanamke mwingine.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment