MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG
ZAWADI UFANYA MAPENZI KUWA MATAMU

Jenga tabia ya kumnunulia zawadi mpenzi wako hata kama ndogo urudipo kazini. Natambua hali zetu za kiuchumi ni duni sana, lakini jitahidi basi urudi hata na Bigijii ya shilingi 50. Ukifika nayo nyumbani mwambie mamaa hii ni zawadi yako spesho.
 

Kwa wale wenye simu, usiache kumpigia simu mkeo mara kwa mara wakati ukiwa mbali naye.
Kwa mfano, kama unaondoka mapema kabla yeye hajanywa chai, ukijua huu ndio muda wa chai basi mpigie simu umuulize kama ameshakunywa chai, akisema bado mhimize aache kwanza kazi ili anywe chai, ikifika wakati wa chakula cha mchana mpigie tena, muulize kama ameshakula, akisema bado mwambie ale ili nawe upate kula huko uliko, mwambie bila yeye kula wewe chakula hakipiti.
Huku ndiko kujenga mapenzi ya dhati, na hii ndio Limbwata Spesho.


Tafadhali hasira zako za kazini usizipeleke nyumbani, yawezekana umekwaruzana na mtu iwe ofisini au hata kwenye daladala, jitahidi hasira ziishie huko huko.
Ukifika nyumbani kama mama yupo kuwa mchangamfu na mwenye utani mwingi wa kimahaba, kwamfano unaweza kujifanya huwezi kuvua tai, koti, shati ama hata viatu na unataka yeye akusaidie kuvua.

Mama akichelewa kukuandalia chakula au maji ya kuoga usiwe mkali, kama tayari Mwenyezimungu amewajaalia mtoto, ukifika usijifanye hujui kulea, mchukue mtoto japo kwa dakika chache huku ukimpa pole mama kwa ulezi wa mchana kutwa.
 

Mankuli (chakula) kikiwa tayari usithubutu kula peke yako. Inawezekana mama akawa amenuna au ameshakula na akakuambia ameshiba, kwakuwa nia yako ni kujenga mapenzi ndani ya ndoa, kataa kula peke yako, mwambie bila kula na yeye huwezi kushiba hata kama utamaliza jungu zima.



Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment