MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG
Kwa mwenye mpenzi mpya

Kuna mambo mengi ya kuzingatia wakati ukiwa na mpenzi
wako siku ya kwanza. Kati ya mambo hayo leo
nitayaelezea mambo 4 tu, ambayo unapaswa kuyaepuka au
 kuyazingatia siku hiyo.

(1)             Chagua maswali ya kuuliza
Ili kutaka kuzifahamu mapema tabia za mpenzi mpya, 

“Hivi umeshawahi kuwa na wapenzi wangapi kabla yangu?
 Unanilinganisha vipi mimi na wapenzi wako walionitangulia?
Kuna ambaye bado unamkumbuka kutokana na mapenzi
yake kwako na jinsi ulivyompenda?”

Maswali haya na mengine mfano wa haya hayaonyeshi
 kujiamini kwako. Haya ni maswali yasiojenga penzi bali
hubomoa. Mpenzi wako hatakusifia kwa maswali haya bali
 atakuchukia.

Kwa vyovyote iwavyo, huwezi kupata majibu ya maswali
hayo kwa kumuuliza mwenuyewe, tena kabla hata hamjazoeana.
Baada ya kujenga upendo utajenga chuki na kuhatarisha hata
 hilo penzi jipya.

(2)             Usimsifie wala kumponda mpenzi wa zamani
Wapo baadhi yetu wanaofikiri ukisifia mambo mazuri uliyokuwa
 unafanyiwa na mpezni wako wa zamani basi huyu wa sasa ndio
atakupenda zaidi na kukufanyioa mambo mazuri zaidi. Si kweli.

“… alikuwa ananipenda sana na hata mimi nilikuwa nampenda,
yaani tulikuwa tunapenda. Alikuwa ananifanyia mambo mengi
mazuri.” Hutakiwi kuzungumza maneno haya mbele ya mpenzi
wako mpya, utaharibu uhusiano wako.

“Unajua alikuwa anajua mapenzi bwana! Alikuwa ananijali na
kunithamini kupita maelezo.” Maneno haya ni sumu katika penzi jipya.

Si kumsifia tu mpenzi wa zamani – hata kumponda mbele
ya mpenzi mpya haifai. Usiwe na tabia ya kumkashifu mpenzi
wako wa zamani hata kama alikuwa na mapungufu yake.
 Acha kutoa siri zake kwa mpenzi mpya kwa kuwa naye hatakuamini.

Ukianza kutoa siri za kashfa za mpenzi wako wa zamani
hutajenga imani kwa mpenzi mpya. Ataamini naye siri z
ake utazitoa nje kama unavyofanya kwa mwenzake. Utakosa
mwana na maji ya moto. Funga domo. 

(3)             Acha kujisifia
Kuna wanaopenda kujisifu na kujikweza ili waonekane
bora mbele ya wapenzi wao wapya. Kuna msemo wa
wahenga waliosema “kizuri chajiuza na kibaya chajitembeza.”

Ubora wa mtu unatokana na vitendo vyake si maneno.
Huna haja ya kuhubiri uzuri wako, wema wako au uwezo
wako wa “kucheza rumba” kwa mpenzi wako, yeye
mwenyewe atang’amua ubora wako baada ya kuwa nawe
kwa muda.

Tabia ya mtu ni sawa na mapembe - haifichiki. Kama
wewe ni hodari wa “ndomboro” atakuona tu bila
hata kujielezea. Tulia aone mwenyewe.    

(4)             Fanya unaloweza
Usifanye kitu kwa kujilazimisha. Hakuna kuigiza kwenye
mapenzi, fanya kile unachoweza na usichoweza kiache.
Kuigiza katika mapenzi ni miongoni mwa sumu zinazoteketeza
upendo wa dhati.

Kwanini? Kwa sababu leo unaweza ukafanya jambo
fulani la kumfurahisha mpenzi wako, lakini umeigiza.
Umejilazimisha kufanya ingawa si fani yako. Umejitutumua
kulifanya ingawa lipo nje ya uwezo wako. Sasa balaa
 litakuja wakati mpenzi wako atakapotaka urudie tena
kufanya hivyo, utashindwa kwa kuwa awali ulijilazimisha.
         
Mfano; kuna wanaume waliotayari hata kukopa au kuazima
 ili kuwaonyesha wapenzi wao wapya kama wanazo, ambao
hawawajui kwa undani.
Wapo wengi wanaoazima magari na ‘pamba’ kwa ajili ya
kutongozea? Utaumbuka.

Si kuazima magari na nguo tu, bali hata mambo mengine
usijilazimishe kufanya ikiwa yapo nje ya uwezo wako.
Kuna wanaopata shida kujilazimisha kufanya hata yale
mambo ya kitandani. Fanya unaloweza na kumuonyesha
 uhalisia wako mpenzi.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment