MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG
USHAURI  
Kuwa mfano wa kuigwa

KARIBU msomaji wa safu hii ya kujuzana masuala mbalimbali
yahusuyo maisha katika familia zetu. Katika safu hii,
 tunazungumza kuhusu mapenzi yanayoweza kuimarisha ndoa
pamoja na malezi bora ya familia.
 Jumatano ya leo tuna mada inayohusu mtu anavyopaswa
kuishi katika jamii yake. Maisha ya ndani kwake, akiwa na
mkewe au mumewe na watoto wake, na pia maisha ya
mitaani akiwa na jamii inayomzunguuka.
Kuna baadhi ya watu wanaishi kwa kutolewa mifano mibaya
 kutokana na vitendo vyao. Ndani ya nyumba zao hawaishi
 kwa amani, mitaani nako kila wanakopita wananyooshewa
 vidole kwa vitendo vyao viovu.
Maisha ya watu wa aina hii ni maisha ya mikasa, na mara zote
hudharaulika katika jamii. Wenye ndugu ambaye anasemwa
vibaya katika jamii wakati mwingine wanajuta kuwa na ndugu
 wa aina hiyo.
Hata mtoto mwenye mzazi ‘kituko’ huona aibu mbele za
 watoto wenziwe anaposikia vituko vya mzazi wake.
Unatakiwa utende matendo mazuri ili uwe kielelezo cha
watu wengine kutenda mema. Kuwa mfano wa kuigwa
katika jamii yako kwa kutenda matendo yatakayowapendeza
wengi. Usiwe mfano mbaya kwa kutenda matendo yatakayo
wachukiza wengi.
Ishi ili watu wengine waige maisha yako. Hata watoto wadogo
ambao hawajayaanza maisha wasemezane wenyewe miyoyoni
mwao kwamba, waishi kama wewe watakapokuwa wanajitegemea.
Kuwa na ndoa yenye mfano wa kuigwa. Wapo baadhi ya
 watu hawatamani kuingia kwenye ndoa kutokana na kuwaona
wazazi wao au ndugu zao na watu wengine wanavyopata
shida kwenye ndoa zao.
Ndoa hazina amani. Hajulikani nani mwenye mamlaka yapi
ndani ya nyumba. Mke na mume hawaheshimiani. Matusi na
 ngumi ndio staili ya maisha yao. Watoto nao wanaunga
mkono mzazi mmoja na kumchukia mwengine wanayefikiri
ndiye chanzo cha migogoro.
Kwa kuwa watoto wanashuhudia ‘mitulinga’ ya wazazi wao kila
siku nao wanajifunza, na ndivyo watakavyokuja kuishi na
 familia zao wakati wao utakapowadia.
Ndugu yangu, usiishi kwa kutolewa mifano mibaya. Ishi kwa
upendo na familia yako ili watu wengine watamani amanai iliyopo
ndani mwenu.
Mpende na muheshimu mkeo. Mpende na muheshimu mumeo.
 Pendaneni na heshimianeni ili watu wengine wawaseme kwa kuwaonea wivu.
 Msiishi maisha yatakayowafanya watu wengine wawaseme kwa
 kuwaonea huruma. Huo ni mfano mbaya katika jamii.
Lea vizuri watoto wako wawe na tabia njema ili wazazi wengine
waige kutoka kwako. Wafanye watoto wako wawe mfano nzuri wa
kuigwa shuleni na hata mtaani. Watu wengine wawaseme watoto
wako kwa kuwatolea mifano mema na hata watamani watoto wao
wawe kama wako.
Si wazazi tu, hata mtoto unatakiwa uishi kwa wema katika jamii.
Penda masomo kwa bidii. Heshimu wakubwa na wadogo.
Epuka vijiwe vya kihuni ili uwe mfano kwa watoto wenzio.

Tabia nzuri kwa mtoto ni chanzo cha mafanikio mazuri ya
maisha ya baadaye. Ukiwa na tabia njema maana yake
utakuwa msikivu kwa wakubwa zako. Utakuwa msikivu na
mtiifu kwa walimu na hivyo ni rahisi kufanikiwa katika masomo yako.
Ishi kwa wema ili uwe mfano wa kuigwa.


Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment