Usipokuwa muwazi utakuwa
mtumwa!
Ndiyo! Pamoja na uvumilivu, mapenzi yanahitaji uwazi,
ukweli, heshima, thamani na uaminifu. Penye upungufu wa
moja kati ya hayo
lazima ndoa itayumba na pengine kuvunjika.
Katika makala yangu ya leo nitazungumzia uwazi katika
mapenzi. Hili ni tatizo
linalowakumba watu wengi katika
ndoa na kusababisha migogoro isiyokuwa ya
lazima.
Kuna sababu nyingi zinazowafanya wapenzi wasiwe wawazi
kwa wenza wao. Nikizitaja kwa uchache ni pamoja na ukali wa
mmoja kati ya mume
au mke, unyonge kwa mmoja
wapo na kutoambilika kwa anayepewa ushauri.
Unaweza kuwa na jambo moyoni linalokuudhi lakini
ukashindwa kumueleza mpenzi wako kutokana na tabia
yake ya ukali, au kwa sababu
hashauriki. Kwa kuwa wewe
huridhiki na mwenendo wake lazima utabaki kuumiza
moyo.
Huo ni utumwa.
Wakati mwingine si kwa sababu mpenzi wako ni
mkali au
haambiliki, ila wewe mwenyewe tu umejiweka
kinyonge zaidi. Unaumia lakini
kusema huwezi hata kwa
yale mambo ya msingi na bahati mbaya mwenzio
hafahamu kama anachokifanya huridhiki nacho.
Anaendelea huku wewe
ukijiweka utumwani.
Tazama ndoa zote ambazo hazina uwazi kwa wahusika.
Awe
mke ama mume asipokuwa muwazi wa kumweleza
chonchote asichokipenda au kutaka
anachokipenda
utagundua kuna minyukano ya ndani ya nafsi kwa wahusika.
0 maoni:
Post a Comment