Siri za ndoa hazitolewi ovyo jamani…
Baada ya kupata maelezo
ya wasomaji wangu nimegundua jambo moja baya kwa wanandoa. Kutoa siri za ndoa
zao. Hilo ni jambo baya na ni aibu kwako unayetoa siri za ndoa yako.
Watu wengi (hasa
wanawake) huwa wanapenda kutoa nje siri za ndoa zao. Kila kinachofanyika ndani
ya nyumba, iwe sebuleni, chumbani au hata kitandani kinasimuliwa kwa watu
wengine wasiohusika.
Kwa maana hiyo, nimeona
bora Alhamisi ya leo ninawakumbushe wanandoa kuzingatia kuficha siri za ndoa
zao. Si jambo zuri hata kidogo kwa mtu kuyazungumza mambo ya ndani ya ndoa yake
kwa mtu mwingine asiyehusika.
Naomba nieleweke vizuri
hapa; sisemi watu wasieleze matatizo yaliyopo ndani ya ndoa zao. Hapana! Na
ndiomaana makala ya wiki iliyopita iliwazungumzia wasuluhishi wa ndoa kwa
kuelewa matatizo yapo na mengine hayavumiliki.
Bila matatizo kwenye
ndoa na mwanandoa mwenyewe kueleza matatizo yake hakuna msuluhishi. Lakini si
kila tatizo linalipaswa kuelezwa au kutafutiwa msuluhishi.
Kibaya zaidi wapo
wengine ambao hutoa nje hata yale mazuri yanayofanyika kwa furaha na kwa
makubaliano yao wenyewe. Wanawaeleza marafiki zao ambao wengi wao hawana msaada
wowote katika kujenga au kuimarisha ndoa.
Kama matendo ya mwenzio
ndani ya ndoa yamekuchosha na unahitaji msaada wa nje, lazima uchague wa
kumweleza ambaye unahakika ataweza kuleta manufaa kwako.
Si kila mtu ambaye
ladba unamuheshimu au kumpenda sana akaweza kukushauri vizuri katika masuala ya
ndoa. Ndiomaana kuna watu maalumu wenye kazi hiyo kama washenga, wazazi na hata
viongozi wa dini. Hawa ndio watu wa kwanza tunaoshauriwa kuwaeleza matatizo
yetu ya ndoa.
0 maoni:
Post a Comment