kutoa ushauri kwa uma.
Naitwa Mama wawili, naishi Mwanza. Nilitokea
kupendana na baba mmoja wa Dar es Salaam ambaye
alikuja Mwanza kikazi.
Tulipokutana tukaanza kupendana na mapenzi yetu
yalikuwa ya dhati yakijumuisha habari za maisha.
Alinisaidia kila kitu nitakacho na aliahidi tutaoana.
Cha kusikitisha ni tangu aondoke Mwanza, mawasiliano
yetu yamekuwa si mazuri. Kila nikimpigia simu anatoa
maneno mawili na kukata simu. Lakini nikimuomba
anitumie vocha katika simu yangu, ananikubalia lakini hatumi.
Naomba ushauri Uncle Jay, niachane naye au
niendelee kuvumilia mpaka nione mwisho wake?
JIBU: Ingawa kuna msemo wa wahenga usemao ‘mvumilivu
hula mbuvu’ inapasa pia tukumbuke na mwingine usemao
‘fimbo ya mbali haiuwi nyoka’.
Kwanza kabla ya kuzama kwenye penzi la baba wa
ungekuwezesha kufahamu alivyo. Anatoka Dar kweli?
Anahitaji kweli penzi lako au anakusudia kukutumia tu
kwa muda?
Inawezekana ana mke na kuwa vigumu kuongeza mwingine.
Pengine alikuwa na shida yake ya muda tu lakini alilazimika
kukudanganya akijua utamuamini.
Hupaswi kujiumiza sana kumfikiria mtu usiyemfahamu
kwa undani. Huyo atakusumbua bure na kwa hakika
anakucheka kuwa hujafahamu mambo.
Achana naye, fanya shughuli zako za kutafuta maendeleo
badala ya kutumia muda mwingi na mawazo yako kumfikiria.
Anakupotezea muda bure.
Nahisi mpenzi wangu kapunguza upendo
Habari ya kazi Uncle Jay? Mimi ni msichana wa miaka 21,
nina mpenzi wangu anayesoma Chuo Kikuu cha
Lakini nina wasiwasi kuwa mpenzi wangu huyu amepunguza
mapenzi kwangu kwa sababu si kawaida yake kukaa wiki bila
ya kuwasiliana nami.
0 maoni:
Post a Comment