MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Hatua mbili muhimu za
kupata mchumba bora

ASALAM alaykum wapenzi wasomaji wangu popote
mlipojaaliwa kupia blog hii ya
MWERAAMAZING.BLOGSPOT.COM
Kama kuna mtu unataka kuchunguza tabia
zake ili aweze kuwa mumeo au mkeo,
huna budi kufanya yafuatayo ili usipate
mke au mume wa ‘bandia.’


ORODHESHA VIGEZO VYAKO
Umefikia umri wa kuoa au kuolewa? Je,
 tayari umeamua kutafuta mchumba ili
mwishoe awe mkeo au mumeo?

Kama majibu ya maswali hayo ni NDIYO,
basi kwanza orodhesha vigezo vya mchumba unayemtaka.


Fanya hivi; chukua peni na karatasi.
Jifungie chumbani peke yako. Andika
sifa za mke au mume unayetaka kuwa naye
kwa kuanza na zile sifa unazodhani kuwa ni
 muhimu kwa kuzipa namba.

Ukimaliza jiridhishe kwa kuzipitia mara ya pili na tatu.
Ukimaliza weka mahala pazuri karatasi yako bila
kumwambia mtu yeyote. Kaa siku tatu ukiipitia
 karatasi yako na kama unaona kuna sifa umeiweka
 lakini haina umuhimu itoe au kama kuna sifa
 unafikiri umeisahahu iweke.


Kama wewe hujawahi kuoa au kuolewa,
 mtafute mtu unayemuamini mno, ambaye
 tayari ameshawahi kuingia kwenye ndoa,
akiwa mzazi wako itakuwa bora zaidi.
Muonyeshe orodha ya vigezo vya mchumba
 unayemtaka. Mwambie akushauri kuongeza vigezo au kuondoa.

Katika sifa unazotakiwa kuziweka, tafadhali
sifa ya utajiri usiipe kipaumbele kwenye mapenzi ya ndoa. 



Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment