AMISOM ITAUHAMA UWANJA WA MOGADISHU
Kikosi cha amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM, kimekubali ombi la
Shirika la Kandanda la Somalia kuhama kutoka uwanja wa mpira wa Mogadishu,
ili uwanja huo upate kufanyiwa ukarabati kuweza kutumiwa tena kama pahala pa michezo.
Mogadishu stadium
Msemaji wa AMISOM, Kanali Ali Adan Hamud, alisema AMISOM imekaribisha ombi hilo na
kwamba AMISOM imeamua kuondoka kwenye uwanja huo ufikapo mwezi wa Disemba
mwaka huu.
Uwanja huo umekuwa kambi ya askari wa AMISOM tangu Agosti mwaka jana.
Kabla ya hapo ukitumiwa na wapiganaji wa Al-Shabab na mapambano makali yamewahi
kutokea kwenye eneo la uwanja huo.

0 maoni:
Post a Comment