RWANDA YASITISHIWA MSAADA
Uingereza imesitisha kwa muda msaada
iliyokuwa iipe Rwanda kwa sababu ya wasiwasi kuhusu kuhusika kwa nchi hiyo
katika mzozo uliopo Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mawaziri walisema kwamba Uingereza
sasa haitatoa msaada wa pauni milioni 21.
Rwanda ilipewa msaada wa kiasi cha
pauni milioni 16 mnamo mwezi Septemba, hata baada ya tashwishi kuwepo kuhusu
tetesi kwamba ilikuwa inawaunga mkono wanamgambo wa M23 wa Jamuhuri ya
Kidemokrasia ya Congo.
0 maoni:
Post a Comment