MARIO BALOTELL KUIPINGA MAAMUZI
Mshambulizi wa Manchester City Kutoka
Italia, Mario Balotellu, atafika mbele ya kamati maalum ya shirikisho la mchezo
wa soka nchini England siku ya Jumatano.
Balotelli
anapinga uamuzi wa klabu yake ya Manchester City ya kumpiga faini ya mshahara
wake wa wiki mbili kuhusiana na rekodi yake mbovu ya nidhamu.
Mchezaji huyo
mwenye umri wa miaka 22, alikosa mechi 11 za ligi kuu na michuano ya ulaya
msimu uliopita.
Balotelli
alikata rufaa kuhusu aumuzi huo, lakini kamati huru ya wanachama wa bodi ya
wakurugenzi wa klabu hiyo wakaifutilia mbali.

0 maoni:
Post a Comment