KIKOSI CHA ZANZIBAR CHAFUNGIWA
Shirikisho la mchezo wa Soka
visiwani Zanzibar,ZFA limechukua uamuzi ambao umewashngaza sana mashabiki wengi
wa soka, visiwani humo, nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Kwa mujibu wa ripoti maafisa wakuu wa ZFA wamewapiga
marufuku wachezaji wake wote walioshiriki katika michuano ya kuwania kombe
CECAFA Senior Challenge, iliyokamilika nchini Uganda, kutoshiriki katika mechi
yoyote popote duniani kwa muda usiojulikana.Aidha ZFA limeamua kuvunja timu ya taifa maarufu kama Zanzibar Heroes, licha ya kuwa timu hiyo ilimaliza katika nafasi ya tatu katika michuano hiyo ya CECAFA.
Baadhi ya wachezaji hao waliopigwa marufuku ni pamoja na nyota na naodha wa Yanga, Nadir Haroub.
0 maoni:
Post a Comment