SYRIA YATUMIA MABOMU
Maafisa kutoka Marekani na shirika
la kujihami la NATO wanasema jeshi la Syria limekuwa likifyatua makombora ya
masafa mafupi katika vita dhidi ya waasi, huku mzozo nchini humo ukizidi
kuzorota.
Maafisa hao, ambao hawakutaka
kutajwa, wanasema makombora hayo, yanofanana na yale ya Scud, yalifyatuliwa
kutoka Damascus hadi maeneo ya kaskazini yanayodhibitiwa na waasi.
![]() |
| MABOMU |
Msemaji mmoja wa Wizara ya Nchi za
Kigeni wa Marekani, Victoria Nuland, alisema serikali ya Syria inatumia silaha
hatari.
Ingawaje alisema kuwa hatatoa
"habari za kinaganaga kuhusu makombora hayo", alithibitisha kwamba
"hivi majuzi ufyatuliaji wa makombora ulikuwa umeonekana".

0 maoni:
Post a Comment