SHIRIKISHO la Soka Barani Africa
(CAF), linatarajia kutuma mjumbe wake kwa ajili ya kuja kukagua klabu zote
zinazoshiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa ajili ya kupewa leseni za
kushiriki michuano ya CAF.
Akizungumza na waandishi wa habari
Dar es Salaa jana, Afisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Bonifasi
Wambura, alisema mjumbe huyo kutoka CAF atafika nchini Januari 7 kwa ajili ya
kufanya ukaguzi huo.
“Ili klabu iweze kupewa leseni ya
CAF kwanza klabu inatakiwa iwe na viongozi walioajiriwa, iwe na uwanja wake wa
mazoezi pamoja na anuani pamoja na ofisi ya klabu pamoja na programu za vijana
,” alisema Wambura.
Wambura pia alisema kwa klabu za
Simba na Azam ambazo zinashiriki katika michuano ya Klabu bingwa Afrika na
Kombe la Shirikisho zenyewe zinatakiwa kuonyesha hotel zitakazotumiwa na wageni
wao wakati wa michuano hiyo.
Mjumbe huyo kutoka CAF anatarajiwa
kuanza kazi hiyo Januari 7 hadi 14 mwakani.
0 maoni:
Post a Comment