MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Uongozi unaosimamia ubereshaji wa mazingira maeneo ya nyanda za juu kusini mwa Tanzania umezungumzia tatizo la uharibifu wa mazingira lililokithiri kwa kiwango kikubwa hapa nchini.
Hayo yamesemwa na maratibu wa kuboresha mazingira nyanda za juu kusini mwa Tanzania Godwell Ole Meing’ataki wakati akizungumza na nuru fm ofisini kwake na kusema kuwa Tatizo hilo katika maeneo ya hifadhi za taifa kama Hifadhi ya Ruaha, limekithili na kupelekea mazingira kuwa kame.
Aidha pamoja na hayo Meing’ataki amesema kuwa tatizo hilo linapelekea kutoweka kwa uoto wa asili,kupungua kwa wanyama kwenye hifandhi za taifa na watalii kupungua katika maeneo ya hifadhi.
Amehitimisha kwa kutoa wito kwa wananchi walioyazunguka maeneo hayo kushirikiana na mamlaka husika katika utunzaji wa mazingira ili kuongeza pato la taifa kupitia sekta ya utalii.

Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment