KIMONDO CHA KIPEKEE DUNIANI KIPO MBEYA
Hakika Watanzania wanatakiwa kuthamini vivutio vyao kwa kuwa katika kituo cha pekee duniani ambacho kimetokea Tanzani ni Kimondo ambacho ni cha nane duniani kwa ukubwa wa tani 12 lakini ni cha kwanza duniani kwa kusheheni madini ya Chuma kwa asilimia 90.5/
Kimondo hicho ambacho kinadaiwa kuanguka katika Kijiji cha Ndondowezi, kata ya Mlangali wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya, zaidi ya miaka 1000 iliyopita.
Hata hivyo kiligunduliwa na Mhuzi kutoka Zambia miaka ya 1930, ambaye alikaribishwa na Chifu wa eneo hilo.
Aidha inadaiwa Wajerumani walipogundua kimondo hicho, walienda kukifanyia utafiti na kubaini kuwa kweli ni Komondo kama ilivyokuwa inasadikiwa.
Kiujumla Kimodno hicho kina kipo mithili ya jiwe, ndani yake kina madini ya chuma, nickel na madini mengine lakini kikigongwa kinatoa mlio wa kipekee mithili ya debe tupu.
Hiki ndicho kimondo pekee kikubwa Afrika na cha 8 duniani |
picha inayokionesha kimondo kwa ukubwa wake |
kimondo |
Mhifadhi wa mambo ya kale msaidizi, Bw. L.H.Napunju, akiwa juu ya kimondo hicho huku akiwapa maelekezo wanafunzi wa DSJ |
0 maoni:
Post a Comment