WATU 185 WAUAWA NCHINI NIGERIA
Zaidi ya raiya mia moja na themanini na tano wamefariki huku nyumba elfu mbili zikiharibiwa kutokana na mapigano makali kati ya jeshi na wapiganaji wa Kiislamu kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Serikali ya mji wa Baga na Ofisa Serikali hiyo Bwana Lawan Kole.
Jeshi na maafisa wa serikali wanasema kuwa kulikuwa na mashambulizi ya gurunedi, zilizosukumwa na roketi na makabiliano ya risasi katika mji tulivu wa Baga unaopakana na Chard Ijumaa jioni.
0 maoni:
Post a Comment