WANANCHI ELFU KUMI KUTEMBELEA MSITU WA SHENGENA
ASASI ya Kiraia ya Mohispac Foundation kwa
kushirikia na uongozi wa mkoa wa Kilimanjaro inatarajia kuandaa matembezi makubwa
yenye lengo la kuhifadhi mazingira na kuokoa msitu wa Shengena na vyanzo vya maji vilivyopo katika msitu huo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana, Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo, Mchungaji Nziacharo Makenya,
alisema matembezi hayo yanayotarajiwa kufanyika Julai 15 mwaka huu yataanzia
Mpinji kuelekea Mamba Miamba.
Alisema matembezi hayo yanakusudiwa kuwa
na viongozi mbalimbali wa kiserikali, mashirika na wadau mbalimbali wa
mazingira pamoja na wananchi waliozunguka maeneo hayo wakiwemo watu wa Chome, Suji, Kirangare Vugwama,
Bwambo Mpinji, Mamba miamba, Lugulu.
“Wengine ni wakazi wa Bombo, Vuje, Mbaga,
ndungu, Kihurio, Gonja, Kisiwani sehemu
nyingi ambapo zaidi ya watu 10,000 watashiriki.
“Pia tunampongeza Mkuu wa Mkoa wa
Kilimanjaro kwa kazi nzuri na njema anayoifanya natimu yake ya kunusuru msitu huo
na kurejesha uoto wa asili ya msitu wa
Shengena.
“Pia tunatambua jitihada zinazofanywa na Mbunge wa jimbo la Same Mashariki, Anna
Kilango, ambazo pia tumeona tuungane nae
katika kampeni hiyo njema ya kulinda, kuhifadhi na kuokoa mstitu huo kwa vyanzo
vya maji na maendeleo yetu,”alisema Makenya.
Alisema wamependa jitihada zinazofanywa
na Serikali na wameamua kuwaunga mkono kwa matembezi hayo ya mazingira hasa
katika msitu huo.
Alisema pamoja na kuwepo utajiri katika
msitu huo lakini upo hatarini kupotea kutokana na uharibifu wa mazingira
unaotishia uhai wa watu na viumbe hai kama ukataji miti ovyo, uchomaji moto uchimbaji
wa siri wa madini unaofanyika ndani ya
msitu huo.
Alisema pia mito mikuu ambayo inaanzia Shengena
ipo hatarini kukauka kama vile mto Nakombo, Hingilili, Yongoma,na Saseni ambayo
hutegemewa kwa shughuli za kilimo katika bonde la Mkomazi ambapo ya ekari 20000
hutumia mito hiyo mikuu kwa kilimo cha mpunga.
Alisema lakini kwa sasa mashamba mengi
hayalimwi kwa sababu ya upungufu wa maji unaofanywa na watu wachache wasiopenda
maendeleo ya msitu huo na mito hiyo.
0 maoni:
Post a Comment