RAIS KENYATTA,
AWATAKA WABUNGE KUTII SHERIA
Rais
Wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa kauli kali kupinga hatua ya wabunge wa Kenya
kutaka kujiongezea mishahara. Rais Kenyatta amesema kuwa taasisi zote za
serikali na afisi zingine zote za umma zitafuata mapendekezo yaliyotolewa na
tume ya kudhibiti mishahara bila upendeleo wowote.
Wabunge wa Kenya wamekuwa
wakilumbana na tume hiyo wakidai imewanyanyasa kwa kuwapunguzia mishahara yao.
Kenyatta emesema malumbano kati ya
wabunge na tume hiyo imelemaza kazi za serikali na kwa hilo rais Kenyatta
emewataka wabunge kukomesha kero zao kwa kushirikiana na tume ya kudhibiti
mishahara ili kuelezea malalmiko yao kwa kufuata sheria.
0 maoni:
Post a Comment