Watu waliokuwa
wamejihami kwa bunduki wamewaua watu 48 katika shambulizi dhidi ya kijiji
kimoja katika jimbo la Zamfara.
Watu hao waliwasili
kabla ya macheo wakiendesha pikipiki.
Baadaye walikwea mlima
uliokuwa karibu na kijiji hicho na kuanza kuwafyatulia watu risasi kiholela
nyumba hadi nyumba.
Shambulizi hilo
linasemekana kuhusishwa na mgogoro kuhusu wizi wa Ng'ombe katika jimbo la
Kaskazini . Kulikuwa na mashambulizi kama haya mwaka jana.
Jimbo lenye idadi
kubwa zaidi ya watu pamoja na kuwa inazalisha mafuta, pia linakabiliwa na
tatizo la makundi ya wapiganaji wa kiisilamu wanaofanya mashambulizi mara kwa
mara.
Hata hivyo, ghasia za
hivi karibuni haziaminiki kuwa na uhusiano wowote na harakati za wapiganaji wa
kiisilamu wa Boko Haram.
Miongoni mwa waliouawa
ni Chifu, Imamu na kiongozi wa kundi la vijana wanaotoa ulinzi.
Walioshuhudia tukio
hilo walisema kuwa wavamizi waliwasili katika eneo la Kizara kabla ya macheo
wakiwa kwenye pikipiki na kuwa walijipanga kwa mashambulizi kabla ya kuanza
kuwaua wanavijiji.
0 maoni:
Post a Comment