Maduka yanayomilikiwa
na wahindi yamevamiwa katika mashambulizi mjini Kinshasa DRC baada ya kukamatwa
kwa wanafunzi wakongomani nchini India.
Mwandishi wa BBC mjini
Kinshasa anasema kuwa raia mmoja mhindi alijeruhiwa katika ghasia hizo na
anatibiwa hospitalini.
Waandamanaji
walighadhabishwa na hatua ya kukamatwa kwa wanafunzi 21 mjini Jalandhar,
Kaskazini mwa India.
Kuna visa vya
kutofautiana kuhusu sababu za kukamatwa kwa wanafunzi hao na kumekuwa na madai
kuwa polisi wamewadhulumu.
Lakini balozi wa India
katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Ram Manohar, aliambia BBC, kuwa
polisi hawakuwadulumu wanafunzi hao, lakini wakasema kuwa kulikuwa na vurugu
wakati wa maandamano.
Aliongeza kuwa
wanafunzi hao waliachiliwa Jumatano nyakati za mchana.
Naibu waziri wa mambo
ya nje wa DR Congo, alitoa ombi kuwa wanafunzi hao waachiliwe mara moja.
Maafisa wa utawala pia
walitaka wanafunzi hao watibiwe kufuatia madai kuwa waliteswa walipozuiliwa.
Mapema taarifa za
vyombo vya habari zilisema kuwa wanafunzi hao walijaribu kujitoa uhai.
Mwandishi wa BBC,
Emmanuel Derville mjini Delhi, anasema kuwa wengi wa wanafunzi hao,
waliozuiliwa wanatoka Kinshasa, na wako nchini humo kusomea uhandisi na masomo
ya biashara kwa miaka miwili iliyopita.
Kulingana na Polisi,
wanafunzi hao walikamatwa baada ya kuzuka kwa mapigano kati ya makundi hasimu
ya wakongomani baada ya kuzuka mapigano katika kituo cha basi
mjini Jalandhar Jumamosi mchana.
mjini Jalandhar Jumamosi mchana.
Naibu wa polisi mjini
Jalandhar, alisema kuwa wanafunzi hao walimpokonya mkoba wake mwathiriwa mmoja.
Lakini wanafunzi hao
walisema kuwa purukushani lilianza baada ya mwanafunzi mmoja nusura kugongwa na
basi
Baadaye alichapwa kwa
bakora katika kile kilichoonekana kama shambulizi la ubaguzi wa rangi.
0 maoni:
Post a Comment