Rais wa Afrika Kusini
Jacob Zuma amefutilia mbali ziara yake ya kwenda Musumbiji baada ya kumtembelea
hospitalini aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Nelson Mandela. Rais Zuma amesema
kuwa Bwana Mandela yuko katika hali mbali ya afya.
Msemaji wa Zuma Mac
Maharaj amesema kuwa hali yake imedorora zaidi katika saa 48 zilizopita.
Mandela ambaye, ni
rais wa kwanza mweusi wa Afrika Kusini, amelazwa hospitalini tangu tarehe 8
mwezi Juni akiugua maradhi ya mapafu.
Madaktari wanasemekana
kufanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa Mandela anapona.
Vikundi vya watu wenye
huzuni mkubwa kuhusu hali ya afya ya Mandela, walikusanyika nje ya hospitali
alikolazwa, wakiwa na ujumbe wa ugua pole kwa Mandela
Wadadisi wanasema kuwa
wananchi wa Afrika Kusini wanaonekana kuwa tayari kwa habari zozote sasa kuhusu
hali ya Mandela.
"tutasikitika
sana ikiwa tutapata habari za kifo chake, lakini pia tutakuwa tunasherehekea
maisha yake. Amefanya mambo mengi zaidi kwa nchi yetu,'' alisema kijana John
Ndlovu, mwenye umri wa miaka 25.
Zuma alitarajiwa
kuhudhuria mkutano wa marais nchini Msumbiji, hii leo lakini akaamua
kuakhirisha safari yake.
Taarifa kutoka kwa
ofisi yake ilisema kuwa anaendelea kuwapongeza wananchi wa Afrika Kusini wanaoendelea
kuiombea familia ya Madiba.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment