Rais Barack Obama amewasili Senegal katika ziara yake ya
wiki moja barani Afrika na anatarajia kuzuru Afrika Kusini na Tanzania akilenga
kustawisha demokrasia na masuala ya uchumi.
Hii ni ziara ya pili ya Obama barani Afrika tangu achaguliwe Rais mwaka 2008.
Hii ni ziara ya pili ya Obama barani Afrika tangu achaguliwe Rais mwaka 2008.
Hata hivyo ziara yake inatarajiwa
kufifishwa na hali mbaya ya afya inayomkabili aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini
Nelson Mandela. Ikulu ya white house imesema kuwa itategemea uamuzi wa familia
ya Bwana Mandela iwapo Rais Obama anaweza
kumtembelea hospitalini.
Katika mkutano wake wa leo na rais wa
nchi hiyo, Mackey Sall, Rais Obama anatajiriwa kuipa heko Senegal kwa rekodi
yake nzuri ya uthabiti ikizingatiwa iko kwenya kanda yenya misukosuko ya
kisiasa.
Maafisa wa Marekani wanasema kuwa muhimu
katika ziara ya Obama ni kustawisha demokarsia na nchi zote tatu anazotembelea
ziko na demokasria thabiti.
Ni ziara ya pili ya Obama katika bara la
Afrika tangu kuwa rais wa Marekani mwaka 2008
0 maoni:
Post a Comment