Mmoja wa viongozi
wakuu wa al-Shabab nchini Somalia, Sheikh Hassan Dahir Aweys,amekata
kujisalimisha , kulingana na taarifa za viongozi vya kiukoo kwa BBC.
Umoja wa Mataifa
uliripoti kuwa bwana Aweys alijisalimisha kwa maafisa wa usalama nchini Somalia
baada ya kutofautiana na kiongozi mkuu wa Al shabaab.
Lakini Aweys yuko eneo
la Galmudug akiwa na wapiganaji wake baada ya kuPewa idhini ya kuingia katika
eneo hilo na maafisa wa utawala.
Walikwenda huko kutoka
Mogadishu kuona ikiwa kweli yuko tayari kwa amani.
Aweys anaonekana kama
kiongozi mkongwe wa Al Shabaab na yuko kwenye orodha ya Marekani ya washukiwa
wa ugaidi baada ya kuhusishwa na shambulizi la kigaidi la 9/11 mwaka 2001 .
Habari za
kujisalimisha kwa Aweyes ni ishara kubwa kuonyesha kuwepo mgawanyiko katika
uongozi wa Al-Shabaab.
Wiki moja kabla ya
kuwasili kwake mjini Adado kupitia baharini, kulikuwa na ripoti kuwa mapigano
yalitokea eneo la Baraawe, moja ya ngome kubwa za Al-Shabaab,ambako Aweys
alikuwa anaishi.
Ingawa anajikuta
katika mazingira asiyoyafahamu vyema, kiongozi huyo anaonekana kuchangayikiwa.
Aliwaambia viongozi wa
kikoo waliokwenda kuongea naye kuwa yeye hajajisalimisha na kuwa hayuko tayari
kusafiri kwenda Mogadishu.
Bwana Aweyes amekuwa
akijulikana na UN kama kiongozi mkubwa katika kundi la al-Shabab na Marekani inamfahamu kama gaidi
0 maoni:
Post a Comment