Raia wa Afrika kusini
wamekesha kwa maombi maombi nje ya makaazi ya zamani ya aliyekuwa rais wa taifa
hilo Nelson mtaani Soweto.
Rais Jacob Zuma
amesema kuwa afya ya shujaa huyo aliyepigana dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini
humo inaendelea kuimarika.
Mandela aliye na umri
wa miaka 94 amekuwa hospitalini akiuguwa ugonjwa wa maambukizi ya mapafu.
Awali mwanawe wa kike,
Makaziwe amesema afya ya babaake inaendelea kuwa njema.
Aidha Makaziwe
amevikashifu vyombo vya habari kwa kukita kambi nje ya hospitali alikolazwa
shujaa huyo akisema wanahabari wanapaswa kumheshimu babaake.
Rais Jacob Zuma
alisema Alhamisi kuwa hali ya Mandela iliimarika lakini bado yuko hali
mahututi.
"leo angalau yuko
sawa kidogo kuliko nilivyomwacha jana usiku,'' alisema Rais Zuma baada ya
kuongea na madakatari wanaomtibu Mandela.
Bwana Zuma alifutilia
mbali safari yake ya Msumbiji ili kumtembelea Mandela hospitalini.
Wakati huohuo mwanawe
Mandela Makaziwe alisema Mzee 'bado yupo' na kuwa anaweza kuhisi mtu akimgusa.
kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment