Rais
wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela amerejeshwa hospitalini mara baada ya
kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu kwenye mfumo wake wa kupumua.
Mandela mwenye umri wa miaka 92
aametajwa kuumwa sana lakini akiwa mwenye hali nzuri na amelazwa kwenye
hospitali moja ambayo hakutajwa jina huko mjini Pretoria mapema usiku wa
kuamkia leo.
Aidha msemaji wa rais huyo wa kwanza
mweusi kwenye taifa la Afrika Kusini amesema hali yake ni njema na anaweza
kupumua bila kutumia msaada wa mashine maalumu.
Hi mara ya tatu kwa mwaka huu bwana
Mandela kulazwa hospitalini ambapo aliwahi kugundulika kuwa na ugonjwa wa kifua
kikuu wakati akitumikia kifungo chake cha miaka 27 jela.
Mkewe Bi Graca Machel amehairisha
ziara yake mjini London ambako alikuwa ahudhurie mkutano maalumu na inaaminika
amerejea Afrika kusini kukaa na mumewe.
0 maoni:
Post a Comment