MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Hillary Clinton kutofunguliwa mashtaka?

Nchini Marekani ,FBI wanasema itakuwa si jambo la kupendeza kufungua mashtaka ya jinai dhidi ya Hillary Clinton kwa kutumia barua pepe binfasi kushughulikia taarifa za siri za kiserikali wakati alipokuwa Waziri wa Mambo ya Nje ya Marekani.
Mkurugenzi mkuu wa kitengo hicho , James Comey,amesema mgombea huyo kupitia chama Democrat alifanya uzembe ingawa hakuna dalili ya kufanya makosa kwa makusudi.
Msemaji wa kampeni wa Hilary Clinton, amesema kwamba Hilary ametambua makosa yake na alidhani jambo hilo lilishamalizika.
Lakini mpinzani wake, mgombea kutoka chama cha Republican Donald Trump amesema kwamba Hilarry hakujali usalama wa nchi na kama asiposhtakiwa itaonyesha jinsi gani mfumo ulivyoharibika
WAKATI HUO HUO
Ikulu ya Marekani imesema kwamba rais Barack Obama hatazungumzia uchunguzi wa FBI.Msemaji wa Ikulu ya Marekani amesema kwamba Obama ameweka msimamo huo kwa kuchelea kuonekana anaingilia kati uchunguzi huo.
Lakini katika saa kadhaa za tamko hilo la FBI, Rais Obama alionekana katika kampeni za Hillary Clinton katika jimbo la Marekani kaskazini.
Obama amsema kwamba ana imani na Hilary na kudai kwamba zaidi ya Hilary hajaona mwanaume ama mwanamke anayefaa kugombea nafasi hiyo zaidi Hilary. Mwezi uliopita Obama binafsi alimtangaza kumuunga mkoano Bi Hillary kuwa mgombea urais wa Marekani.

Kutoka BBC Swahili
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment