MWERA AMAZING BLOG

MWERA AMAZING BLOG

Oscar Pistorious kwenda jela


Mwanariadha mlemavu wa miguu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius leo atafahamu iwapo atakwenda jela kwa kosa la mauaji ya mpenzi wake Reeva Steenkamp au la.
Mwanariadha huyo alipatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake baada ya maamuzi ya rufaa dhidi yake ambapo sasa anakabiliwa na kifungo cha miaka 15 jela baada ya vita ya kisheria iliyochukua takriban miaka mitatu.
Mwanariadha huyo Oscar Pistorius tayari ameshatumikia kifungo cha takribani miezi tisa jela katika kosa la awali wakati alipopatikana na hatia ya kuua bila kukusudia mwaka 2013.


Kwa sasa kifungo chake kimeongezeka baada ya upande wa serikali kushinda rufaa hiyo ambapo kosa lake lilibadilika na kuwa kosa la kuua kwa kukusudia.
Hata hivyo katika tukio la aina yake mwezi uliopita wakati wa kusikilizwa kwa shauri hilo kuhusu adhabu aliyopewa mwanariadha alishauriwa na timu ya wanasheria wanaomtetea walimshauri kuvua miguu ya bandia na kutembea kwenye chumba cha mahakama bila miguu hiyo.
Hatua hiyo ya kuvua miguu ya bandia iliyomfanya ashindwe kusimama vizuri ilikuwa na lengo la kumshawishi jaji ili auone udhaifu wake na kuamua ama amhukumu kutumikia jela kwa muda wote huo au la.
Hata hivyo upande wa mashtaka ulitoa hoja na kusema ulemavu mwanariadha huyo si jambo la msingi. Ambapo waliikumbusha mahakama kwamba Oscar Pistorius alimfyatulia risasi mpenzi wake Reeva Steenkamp mara nne alipokuwa amejifungia maliwatoni.
Japokuwa adhabu ya kosa la mauaji ya kukusudia nchini Afrika Kusini ni kifungo kisichopungua miaka 15 jela lakini Jaji Thokozile Masipa anaweza kuangalia kama kuna uwezekano kupindisha kidogo sheria hiyo. Anaweza pia kuzingitia hisia za mlemavu huyo alivyoonekana kujutia kosa lake.
Wanaompinga mlemavu huyo wamekuwa na shaka na uwezekano maamuzi hayo. Wanasema katika mahojiano ya njia televisheni yaliyorushwa wiki mbili zilizopita, Oscar Pistorius amekuwa akifanya maudhi.
Wanasema kama itakuwa hivyo itaonyesha udhaifu hukumu na itakuwa ni matusi kwa mahakama na kwa familia ya Reeva Steenkap ambaye amechukizwa.
kutoka BBC Swahili.
Share on Google Plus

About MWERA AMAZING

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 maoni:

Post a Comment