UINGEREZA YAKUBALI KUWAFIDIA MAU MAU
Serikali ya Uingereza imetangaza
kuwa itawalipa fidia ya dola milioni thelathini manusura wa harakati za
ukombozi wa Uhuru wa Kenya Mau Mau.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza
William Hague ametangaza kuwa serikali yake itawalipa wale wote walioteswa na askari
wa ukoloni katika miaka ya 1950.
Waliokuwa wanachama wa vuguvugu hilo
waliwasilisha kesi mahakamani kwa mateso na dhuluma walizodai kutendewa na
uliokuwa utawala wa ukoloni miaka ya 50.Huenda pia Uingereza itatangaza fidia.
Waliokuwa wanachama wa vuguvugu hilo
waliwasilisha kesi mahakamani kwa mateso na dhuluma walizodai kutendewa na
uliokuwa utawala wa ukoloni miaka ya 50.Huenda pia Uingereza itatangaza fidia.
Zaidi ya wakenya 5,000, waliteswa
baadhi wakinyanyaswa na waliokuwa wakoloni wa Uingereza.
Uingereza ilipigana vita vikali
dhidi ya Mau Mau, waliokuwa wanadai ardhi na kuondoka kwa utawala wa kikoloni.
Baadhi ya waliokuwa wanachama wa Mau
Mau
Manusura wa vita hivyo wamekuwa
wakiidai Uingereza kuwalipa fidia kwa miaka mingi.
BBC ina habari kuwa bwana Hague
atawaomba radhi waathiriwa wa vita vya Mau Mau, wakati akitangaza kiwango cha
pesa watakazotoa kama fidia kwao.
Serikali ya Uingereza awali ilikuwa
imesema kuwa madai yote ya vitedno walivyofanya wakoloni ni juu ya serikali ya
Kenya tangu kuipa uhuru mwaka 1963 na kuwa kwa sasa haiwezi kutakiwa kulipa.
Lakini mwaka 2011, mahakama iliamuru
kuwa, wanaodai fidia, Paulo Muoka Nzili, Wambuga Wa Nyingi na Jane Muthoni
Mara, walikuwa na haki ya kudai fidia kutoka kwa Uingereza .
Mawakili wao wanasema kuwa Nzili
alihasiwa , huku Bwana Nyingi akichapwa vibaya wakati Bi Mara akiteswa
kimapenzi katika kambi za mateso ambako waliokuwa wanapinga ukoloni walikuwa
wakifungwa.
Baada ya uamuzi wa kesi hiyo,
ilirejeshwa katika mahakama kuu ili kuamua pesa watakazolipwa na ofisi ya
jumuiya ya madola.
Mahakam kuu Uingereza iliamua kuwa
walalmishi walipaswa kutendwa haki
Duru zinasema kuwa serikali
ilikumbwa na wakati mgumu kupata mashahidi na stakabadhi muhimu kuweza kuelezea
ukweli katika kesi hiyo.
Lakini Oktoba mwaka jana, mahakama
iliamua kuwa waathiriwa waliowasilisha kesi hiyo mahakamani walikuwa na haki ya
kufidiwa kwani walikuwa na kesi nzito dhidi ya serikali ya Uingereza.
Watatu hao walikuwa wamesema kuwa
wangekubali wahusika wa kesi kuafikiana nje ya mahakama lakini pia walikuwa
wanataka kufuata sheria kwani waliona wangepata haki katika mahakama.
kutoka,BBC
0 maoni:
Post a Comment