FAMILIA
YA PISTORIUS YASHTUSHWA NA PICHA
Familia ya mwanariadha mlemavu
nchini Afrika Kusini, Oscar Pistorius, wameshstushwa na picha zilizofichuliwa
za bafu alimomuulia mpenzi wake mnamo mwezi Februari.
Shirika la habari la Uingereza la
Sky, mnamo Ijumaa, lilionyesha picha za kuogofya zinazoshukiwa kuwa za bafu
ambalo mpenzi wa Pistorius Reeva Steenkamp, aliuawa.
Polisi walisema kuwa wamechukizwa
mno na kufichuliwa kwa picha hizo.
Bwana Pistorius mwenyewe anakanusha
madai ya kumuua mpenzi wake, kupitia mlango wa bafu alimokuwa , alisema
alidhani kuwa alikuwa mwizi aliyevamia nyumba yake.
Anatarajiwa kufikishwa mahakamani
kwa hatua ya mahakama mwanzo kutathmini kesi siku yake Jumanne.
Pistorius ni mwanariadha mlevamu
asiye na miguu yake miwili ingawa hukimbia kwa miguu bandia au vyuma. Alishiriki
michezo ya Olimpiki mjini London mwaka jana.
''Familia ya Pistorius ilimuunga
mkono alipokuwa anajiandaa kufikishwa mahakamani , alisema mjomba wake,''
Arnold Pistorius.
''Tunaamini maneno yake , tunampenda
na tutamuunga mkono kwa kila hatua ya kesi hii,''alisema Mjombake Pistorius.
"tumeshtushwa na picha hizi za
ajali iliyotokea nyumbani kwa Oscar."
Msemaji wa polisi ameelezea kuwa
polisi wanachunguza nani aliyefichua picha hizo .
''Kitendo hiki hakikuhitajika na
kimetuudhi kweli. Hatujui picha hizi zimetoka wapi,'' alisema polisi huyo.
Pistorius atafikishwa mahakamani
Jumanne kwa mara ya kwanza tangu kuachiliwa kwa dhamana, kufuatia kukamatwa
kwake, kuhusu mauaji ya Steenkamp.
Kesi hiyo inatarajiwa kuakhirishwa
kwani uchunguzi wa polisi ungali unaendelea.
Pistorius ameajiri baadhi ya
mawaklili shupavu nchini Afrika Kusini kumtetea.
Anasema kuwa alimpiga risasi Bi
Steenkamp kupitia mlango wa choo kimakosa baada ya kudhani kimakosa alikuwa
mwizi.
Hata hivyo, viongozi wa mashtaka
wanasema kuwa alimuua kwa maksudi baada ya wawili hao kugombana.
0 maoni:
Post a Comment