Takriban waumini 44 wameuawa kwa
kupigwa risasi wakiwa msikitini Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa
maafisa wa jimbo la Borno.
Mauaji hayo yalifanyika wakati wa maombi ya asubuhi Jumapili
, ingawa taarifa zimejitokeza Jumatatu , kutokana na hitilafu ya mawasiliano
kwani jimbo hilo liko chini ya sheria ya hali ya hatari.
Shambulizi lilifanyika katika mji wa Konduga, ulio umbali wa
kilomita 35 kutoka mji mkuu wa jimbo hilo , Maiduguri.
Washambulizi wanasemekana kuwa wanachama wa kundi la
wapiganaji la Boko Haram, ambalo liliwaua maelfu ya watu tangu mwaka 2009.
Gazeti la Daily Post, liliripoti kuwa watu wengine 26
walikuwa wanatibiwa kwa majeraha waliyopata wakati wa shambulizi hilo
hospitalini Maiduguri.
Mwanachama wa kikundi cha vijana kinachotoa ulinzi kwa raia,
aliambia shirika la habari la Associated Press, kuwa wapiganaji wao wannne
waliuawa walipojaribu kutoa kilio cha kutaka usaidizi.
Raia wengine kumi na wawili, waliuawa katika kijiji cha Ngom
kinachopakana na Maiduguri.
Rais Goodluck Jonathan alitangaza sheria ya hali ya hatari
katika majimbo matatu Kaskazini Mashariki mwa nchi mnamo mwezi Mei wakati
wanajeshi walipofanya operesheni dhidi ya wapiganaji wa kiisilamu.
Boko Haram linapigania eneo la Kaskazini mwa nchi likitaka
kujitawala kwa kutumia sheria za kiisilamu.
Mwandishi wa BBC mjini Lagos, anasema kuwa wakati kundi hilo
limekuwa likishambulia makanisa, pia limekuwa likishambulia misikiti.
Habari za mashambulizi hayo zilijitokeza wakati kanda ya
video ya kiongozi wa kundi hilo Abubakar Shekau, ilipotolewa akidai kundi hilo
kuhusika na mashambulizi hayo ikiwemo kushambulizi dhidi ya vituo vya polisi na
kambi za jeshi.
kutoka BBC.
0 maoni:
Post a Comment