AL MARKHIYA SPORTS CLUB
P O BOX 21923
DOHA, QATAR
TANZANIA FOOTBALL FEDERATION
P O BOX 1574
DAR-ES-SALAAM
TANZANIA
YAH: KUOMBA MSAMAHA KWA CHAMA CHA
MPIRA TANZANIA
Husika na kichwa cha habari hapo juu
mimi mchezaji MWINYI KAZIMOTO naomba msamaha kwa kitendo nilichokifanya cha
kuondoka kambini timu ya taifa na kuiacha nchi yangu katika kipindi kigumu hali
ya kuwa walikuwa na mechi ngumu na muhimu dhidi ya Uganda.
Halikuwa lengo langu kuidhoofisha
nchi yangu bali ni tamaa yangu ya kucheza mpira nje ya nchi ndiyo iliyonifanya
niondoke katika kipindi hicho, na nashukuru mungu nimefanikiwa kupata team
nchini Qatar, naamini watanzania wataipokea habari hii kwa vizuri.
Mwisho kabisa napenda kuwahakikishia
watanzania na chama cha mpira kwa ujumla kwamba naahidi nitaitumikia nchi yangu
muda wowote watakaponihitaji.
Natumai chama cha mpira na
watanzania kwa ujumla watanielewa na watanisamehe.
Wenu mtiifu
MWINYI KAZIMOTO
0 maoni:
Post a Comment