Mrisho Ngasa,
ambaye alikuwa akichezea kikosi cha wekundu wa Msimbazi SIMBA SC, kwa mkopo
akitokea katika klabu ya AZAM FC, kwa sasa ametajwa kuichezea Timu ya YANGA,
kwa shalti la kuilipa timu ya Simba fidia ya shilingi Milioni 45, ikiwa
imejumuhishwa na fidia ya asilimia 50.
Kamati pia imemfungia mechi sita za mashindano (kuanzia mechi ya Ngao
ya Jamii), na anatakiwa awe amelipa fedha hizo ndani ya kipindi hicho cha
kukosa mechi hizo. Akishindwa, hataruhusiwa kucheza hadi atakapolipa fedha
hizo.
Kwa upande wa wachezaji wa kigeni, Kamati imeagiza
wasiruhusiwe kucheza hadi watakapopata Hati za Uhamisho wa Kimataifa (ITC)
pamoja na vibali vya kufanya kazi nchini (work permits).
Kamati hiyo itakutana tena Ijumaa (Agosti 23 mwaka
huu) ili kupata ripoti za pingamizi ilizoagiza ziwe zimefanyiwa kazi hadi
Agosti 22 mwaka huu na kutoa uamuzi kwa pande ambazo hazikuafikiana.
0 maoni:
Post a Comment