Msanii wa zamani wa kundi la B2K, mbaye ni
RAZ-B, mwenye umri wa miaka 28, amelazwa hospital hapo jana kutokana na kupata
majelaha katika mdomo wake kufuatia ugomvi uliotokeza katika Club, aliyokuwa
akitumbuiza huko nchini China.
Raz B, aliongea na TMZ, na kusema kuwa wakati
alipokuwa akiimba jukwaani alisikia watu wakipigana ndiyo akashuka jukwaani na
kwenda kuamulia ugomvi huo, kutokana na kitendo hicho jama mmoja akamtupia
chupa na kusababisha majelaha katika uso wake.
Mara baada ya muda Polisi wa nchini China ,
walitokea sehemu ya tukio na kuwakamata wote wawili na kufikishwa katika kituo
cha polisi punde msanii huyo alibainka kuwa hakuwa na matatizo ndipo
alipotolewa na kupelekwa Hospital kwa matibabu.
Raz, alitoa haya
maneno "F**k this s**t hurts. I have a
f**king hole in my lip. Thank god I made it to the hospital." Raz, amekuwa nchini China kwa
kipindi cha miaka 3, na amesema kuwa hana mpango wa kufungua kesi yoyote bali
yuko mbioni kurudi zake nchini U.S, kabla ya mwaka huu kwisha.
0 maoni:
Post a Comment