1. Hivi karibuni tumepata uhakika kuwa Tanzania
Premier League (TPL) na Azam Media wanayo nia ya kuingia mkataba wa kuonyesha
mechi za Ligi Kuu (Premier League) kwa msimu wa 2013/2014, 2014/2015 na
2015/2016
2. Baada ya Kamati ya Utendaji ya YANGA kufanya uchambuzi wa kina juu ya
taarifa ya makubaliano ya kibiashara ya TPL / Azam Media ilihitimisha
kuwamkataba huu hauna maslahi kwa YANGA, na kwa hivyo, Kamati ya Utendaji ya
YANGA ilifikia uamuzi kuwa mechi za YANGAzisirushwe hewani na Azam Media.
Kwa kuwa wawazi,
Kamati ya Utendaji ya YANGA ilitoa taarifa kwa wanachama wa YANGA kupitia
vyombo vya habari tarehe 29 Julai, 2013 ambapo iliweka bayana sababu zake na
kueleza kuwa YANGAhaina tatizo na vilabu vingine vya mpira wa miguu ikiruhusu
mechi zao kurushwa na Azam Television ila haifurahii kuwa TPL inalazimisha
YANGA kuonyesha mechi zake za Vodacom Premier League katika Azam Television.
3. Sote tumeona baada ya hapo kuwa “nguvu ya
ziada” inatumika kupotosha msimamo wa Kamati ya Utendaji ya YANGA na
kuidhalilisha Klabu ya YANGA hadharani.
Juu
ya hayo Na Kwa kushangaza Sana, baadhi ya vilabu vya mpira WA miguu ambavyo
vina sifa kuwa havijawahi kushinda Ligi Kuu, vimeundwa hivi juzi tu, havina
uzoefu wowote WA kucheza soka kimataifa n.k. vina kuja kuyapanga Kamati ya
Utendaji ya YANGA jinsi ya kuendesha shughuli za Klabu ya Yanga, vikiwa
vinasahau vilabu vyao wenyewe na badala yake kuiingilia YANGA kwa sababu
zinazojionyesha wazi.
Inadhihirika
wazi kwamba kuna ushirikiano usio mzuri unaoashiria kula njama kuilazimisha
YANGA iruhusu mechi zake zirushwe na Azam Television.
Kwa
kuwa YANGA ni Klabu ya Wanachama yenye kupata nguvu kutokana na misingi yake ya
kidemokrasia iliyojijengea na uamuzi wake wa mwisho unatokana na Wanachama wake
mwenyewe, umeamua kuliweka suala hili zima kwa Wanachama wa Yanga ili waamue ni
njia gani ya kufuata kwa maslahi ya Klabu yetu.
Kwa
kuzingatia hali hiyo basi, na kulingana na mamlaka niliyonayo kama Mwenyekiti
wa YANGA, natangaza mkutano wa dharura wa Wanachama wa YANGA tarehe 18 Agosti,
2013 utakaofanyika uwanja wa Sabasaba kwenye ukumbi wa PTA saa 3.30 asubuhi
waje tujadiliane na kuamua suala la Azam Television kurusha mechi za YANGA.
(YUSUF MANJI)
MWENYEKITI WA YOUNG AFRICANS SPORTS
CLUB
0 maoni:
Post a Comment