Marekani na Muungano
wa Ulaya wamezitaka pande zote katika mgogoro wa kisiasa wa Misri, kumaliza
mzozo wao unaosemekana kuwa hatari kwa taifa hilo.
Hii ni baada ya
serikali ya mpito kusema kuwa juhudi za mapatano zimekosa kufua dafu.
Katika taarifa yao ya
pamoja, walisema kuwa serikali ya Misri ndio ina jukumu kubwa kuanzisha
mazungumzo na kuhakikisha kuwa mchakato huo unafanikiwa.
Serikali ya mpito
inayoungwa mkono na Jeshi, imesema kuwa jeshi litalazimika kuvunja mkusanyiko
wa wafuasi wa Morsi ambao wamepiga kambi mjini Cairo wakitaka aachiliwe.
Mamia ya watu
wamefariki tangu kuanza kwa vurugu zilizofuata kuondolewa mamlakani kwa Morsi
tarehe 3 mwezi Julai.
Tangu hapo,
wanadiplomasia kutoka Marekani, Muungano wa Ulaya na Milki za kiarabu, wote
wamejaribu kusuluhisha mgogoro huo.
Lakini siku ya
Jumatano rais wa mpito Adly Mansour alitangaza kuwa juhudi za kidiplomasia
zimekosa kufaulu na hivyo kusema kuwa mazungumzo yaliisha hiyo jana.
''Juhudi hizi
hazijaweza kuafikia lolote,'' ilisema taarifa ya rais.
Rais alisema kuwa
analilaumu vuguvugu la Muslim Brotherhood ambalo linamuunga mkono Morsi kwa
kuwa sababu ya kukosa kufaulu kwa mazungumzo.
Kutoka BBC
0 maoni:
Post a Comment