
Mr
Nice,
ameingia tena katika mgogoro na lebo yake ya sasa huko nchini Kenya, inafuatiwa
na kile kinachosadikika kuwa msanii huyo na lebo hiyo kuna baadhi ya mambo
hawakuwa wanakubaliana katika kushauriana.
Mkurugenzi wa lebo ya Candy and candy Records, alisema
kuwa walitofautiana mara baada ya kampuni kutaka kazi zenye ubora kutoka kwa
msanii huyo, aliendelea kwa kusema kuwa Mr Nice, ni msanii anayependwa sana
hasa Mombasa, lakini siku chache zilizopita tulikuwa katika mabishano kidogo
hii ilitokana na mtazamo tofauti hasa ni kutokana na wimbo wake mpya wa Akina
Mama, binafsi ule wimbo sikuupenda na nilimshauri kwamba ni vyema tungetumia
wimbo mwingine, lakini aligoma.
Wimbo huo haukupendwa kabisa na wadau na mashabiki
wa muziki nchini humo, hayo yalikuwa maneno ya meneja wa Mr Nice.
0 maoni:
Post a Comment