
Wabunge wa bunge la waakilishi Nigeria wamerushiana ngumi wakati wa vikao
vya Jumanne baada ya kuzuka bungeni suitofahamu kuhusu mrengo wa wabunge
waliojitenga na chama tawala. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa vyombo vya habari
nchini humo.
Kituo kimoja cha
kibinafsi cha televisheni, pamoja na vituo vingine vilionyesha picha za mbunge
mwanamke akimtosa kidole usoni kwa ghadhabu mbunge mwenzake wakati mbunge
mwanamume akionekana akichukua kiti nusura kumgonga mwenzake.
Wabunge wengine
walionekana wakipigana ngumi.
0 maoni:
Post a Comment